Taarifa iliyonifikia kutokea Mwanza ni
hii ya kusikitisha ya watu watatu kuuawa kwa kuchinjwa wakiwa katika
nyumba ya ibada usiku May 18, 2016, Msikiti wa RAHMAN eneo la Ibanda
relini mtaa wa Utemini Mkolani Mwanza.
Ripoti kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mwanza Ahmad Msangi amesema……Watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia
mavazi ya kuficha uso, wakiwa na Mapanga, Shoka na Bendera nyeusi yenye
maandishi meupe waliingia msikitini wakati waumini wakiwa wanaswali
wakazima taa wakisema Kwanini mnaswali wakati wenzenu wanashikiliwa na
Polisi?’
Msikiti wa RAHMAN ambapo tukio limetokea
‘Waliouawa
1.Feruz Ismail Elias (27) Imamu wa
Msikiti, 2.Mbwana Rajabu (40), 3.Khamis Mponda (28) pamoja na Ismail
Abeid (13) aliyejeruhiwa mwanafunzi wa shule ya Jabar Hila Nyasaka,
anapata matibabu kwenye Hospital ya Nyamagana ;- Kamanda Ahmad Msangi
Waumini wengine walifanikiwa kukimbia
huku wahalifu wakikimbia na kurusha chupa mbili za Konyagi ndani ya
Msikiti zikiwa na Petroli pamoja na tambi moto, chupa moja ililipuka ila
haikuleta madhara makubwa’ Amesema Kamanda Ahmed Msangi