Meneja wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella akiwaeleza kinachoendelea baadhi ya mastaa waliofika msibani hapo.
Mdogo wa marehemu Abdul Bonge, Bab Tale akihojiwa na Mwandishi Mwandamizi na Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Bukos.
Mdogo wa marehemu, Habib Uledi (kushoto) akimueleza jambo msanii wa filamu za Kibongo, William Mtitu.
Mchekeshaji Kitale a.k.a ‘Mkude Simba’ akiingia msibani huku akifuatiwa na mchekeshaji mwenzake, Stan Bakora.
KIFO cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale, kilichotokea Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, jana jioni kimeendelea kuzua utata kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd kuingia mitini.
Akizungumza na mandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe.
Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo
No comments:
Post a Comment